Cleopa Msuya:Serikali inatakiwa Kufikiri Juu ya Kuimarisha Masuala ya Umeme Nchini - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Cleopa Msuya:Serikali inatakiwa Kufikiri Juu ya Kuimarisha Masuala ya Umeme Nchini


Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akiteta na Waziri Mkuu,Mstaafu,Cleopa David Msuya kwenye viwanja vya  Kituo cha mikutano  cha St.Gaspar Mjini Dodoma  May 9,2011, walikohudhuria  Semina Elekezi.
--
WAZIRI Mkuu Mstaafu, Cleopa Msuya ameitahadharisha Serikali kuwa makini na suala la mgawo wa umeme ambao amesema unaongeza ugumu wa maisha kwa wananchi, kwani unaweza kusababisha matatizo makubwa kiasi cha nchi kushindwa kutawalika.“Hali ikiendelea hivi tusishangae kutokea kwa mambo kama yaliyotokea kwa nchi za Kiarabu ambazo wananchi wake wameshindwa kuvumilia ugumu wa maisha na kuamua kuandamana.” Msuya alitoa tahadhari hiyo, Dar es Salaam jana wakati wa mjadala wa kitaifa  kuhusu miundombinu,nishati na madini kwenye Wiki ya Maonyesho ya Miaka 50 ya Uhuru yaliyoandaliwa na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF).

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages