Pichani ni Balozi wa Umoja wa Falme
za nchi za Kiarabu nchini Bw. Mallalla Mubarak Al-Ameri na kiongozi wa
Mabalozi wa Kundi la nchi za Kiarabu akisoma hotuba kwa wageni
waalikwa katika maonyesho ya Picha yaliyofanyika katika ukumbi wa
Diamond Jubilee VIP jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Brazil
nchini Mh. Francisco Luz akizungumza wakati wa kufunga maonyesho ya
"AMRIK" yaliyoandaliwa kwa ushirikiano kati ya Ubalozi wa Brazil,
Taasisi za nchi za Kiarabu na Aga Khan. Ambapo Balozi huyo
amewapongeza walioshiriki maonyesho hayo. Maonyesho hayo yenye lengo la
kuhamasisha ushirikiano kati ya Wabrazil na Waarabu yalitarajiwa
kufanyika wiki iliyopita lakini yakaahirishwa kufuatia ajali ya kuzama
kwa Meli ya MV SPICE ISLANDER iliyotokea huko Zanzibar.Katikati ni
Balozi wa Umoja wa Falme za nchi za Kiarabu nchini Bw. Mallalla Mubarak
Al-Ameri na kiongozi wa Mabalozi wa Kundi la nchi za Kiarabu na
Kushoto ni Mwakilishi wa Mtandao wa Maendeleo kutoka Taasisi ya Aga
Khan Bw. Navroz Lakhani.
Kwa Picha Zaidi BOFYA HAPA
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)