Wachezaji wa Yanga kutoka (kushoto) Julius Mlope, Rashid Gumbo na Nurdin Bakar. |
Viingilio katika mechi ya Ngao ya Jamii (Community
Shield) kufungua msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya
mabingwa watetezi Yanga na Makamu Bingwa Simba itachezwa kesho katika
Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam ambapo viingilio vitakuwa ni kama ifuatavyo:-
Viti vya bluu sh. 5,000, Viti vya
kijani sh. 7,000, Viti vya rangi ya chungwa sh. 10,000, VIP C sh.
20,000, VIP B sh. 25,000 na VIP A sh. 50,000.
Tiketi
zimeanza kuuzwa leo mchana (Agosti 15 mwaka huu) kwenye vituo vyote vya
mafuta vya Big Bon jijini Dar es Salaam. Pia zinauzwa katika baadhi ya
vituo vya Oilcom na TSN.
LIGI DARAJA LA KWANZA
Ligi ya Taifa ngazi ya Fainali
imemalizika jana kwenye Uwanja wa Mkwakwani, jijini Tanga. Timu zilizofanikiwa kupanda daraja la kwanza kwa
kuongoza makundi yao ni Polisi Central ya Dar es Salaam, Mlale JKT ya
Ruvuma na Mgambo Shooting ya Tanga. Timu zilizopanda kama washindwa bora
ni Samaria ya Singida na Small Kids ya Rukwa.
Usajili kwa ajili ya timu za daraja
la kwanza utafanyika kuanzia Agosti 15 mwaka huu hadi Septemba 15 mwaka
huu. Jumla ya timu 18 zitashiriki ligi inayotarajiwa kuanza mwishoni mwa
Septemba mwaka huu. Taarifa rasmi ya tarehe ya kuanza ligi hiyo
itatolewa baadaye.
Timu nyingine za Daraja la Kwanza ni
Temeke United ya Temeke, Polisi (Iringa), Burkina Faso (Morogoro), Polisi (Morogoro), Rhino Rangers (Tabora),
Polisi (Tabora), 94 KJ (Green Warriors) ya Kinondoni,
Tanzania Prisons (Mbeya), Morani (Manyara), Transit Camp (Temeke), Rhino FC (Mbeya), Majimaji (Songea) na AFC
(Arusha).
Manyema Rangers ya Ilala, Nyerere FC
ya Kilimanjaro na Mwanza United ya Mwanza ndizo
zilizoshuka daraja kurudi Ligi ya Taifa.
Boniface
Wambura
Ofisa
Habari Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)