BABA WA OBI ATEKWA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

BABA WA OBI ATEKWA

BABA wa kiungo wa Chelsea, Obi Mikel ametekwa nchini Nigeria na kwa sasa hajulikani yuko wapi, huku watekaji wake wakiwa hawajatoa ombi lolote kama wanataka fedha au la.

Mikel alicheza pambano la Jumapili la Ligi Kuu dhidi ya Stoke City ambapo timu hizo zilitoka suluhu, huku baba yake huyo akiwa ametekwa toka Ijumaa.
Mpaka sasa familia yake haijaambiwa nini ambacho watekaji wanataka na wapi alikopelekwa na mchezaji huyo ameomba baba yake huyo aachiwe.
“Tafadhali naomba mumuachie. Kwanza yeye ni mzee na hawezi kufanya jambo lolote lile na wala sielewi ni kwa nini ametekwa. Baba yake huyo Michael Obi, anaendesha kampuni ya usafiri na alishindwa kurejea nyumbani kutoka kazini kwake kutoka eneo la Jos lililo kwenye Jimbo la Plateau lililo katikati ya Nigeria.
Habari Kwa Hisani Ya Dina Ismail

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages