Wanyange hawa leo watapandaa jukwaani katika shindano dogo la kumsaka
Miss Top Model. Mrembo ambaye moja kwa moja atapata tiketi ya kuingia
nusu fainali za Miss Tanzania.
Warembo
wakiunga mkono hoja kwa kuipigia makofi. Warembo 30 wapo kambini
kwaajili ya kujifua na mchuano huo utakao fanyika mwezi Septemba jijini
Dar es Salaam.
Warembo
wanao wania taji la Vodacom Miss Tanzania 2011, wakifuatilia mafunzo
katika semina maalum ya warembo hao inayoendelea katika Hotel ya Giraffe
Ocean View iliyopo Mbezi Beach jijini Dar es Salaam. Warembo hawa baada
ya kumalizika semina hii watahamia katika Jumba la Vodacom House.
Mkurugenzi
wa Lino International Agency, Waandaaji wa Miss Tanzania, Hasim
Lundenga (katikati) akifafanua jambo wakati wa semina maalum kwa
washiriki wa Vodacom Miss Tanzania 2011. Kulia ni Mkurugenzi wa Ukuzaji
Sanaa kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Nsao Shalua na kushoto ni
Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania Prashant Patel.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)