Ofisa
Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom
Tanzania Mwamvita Makamba akikabidhi sehemu ya sadaka ya futari kwa
watoto wa madrasa za wilayani Mafia yenye thamani ya zadi ya shilingi
milioni tisa. Vodacom kupitia mfuko wake wa kusaidia jamii wa Vodacom
Foundation ilikabidhi sadaka ya futari kwa watoto zaidi ya mia tatu wa
kisiwani Mafia hafla iliyoambatana pia na kufuturisha katika msikiti
mkuu wa Wilaya mwishoni mwa wiki. Wanaoshudia makabidhiano hayo ni Mkuu
wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule na Imam Mkuu wa Msikiti wa
Wilaya Ally Mwabaku.
Wanafunzi
wa Madrasatul Shamsia ya Mjini Mafia wakipokea kwa furaha katoni ya
sabuni kutoka kwa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa kampuni ya Mawasiliano
ya Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba.Vodacom kupitia mfuko wake wa
kusaidia jamii wa Vodacom Foundation ilitoa pia sadaka ya vyakula kwa
ajili ya futari kwa wanafunzi zaidi ya mia tatu wa madrasa mbalimbali
wilayani humo pamoja na kuwafuturisha mwishoni mwa wiki.Wanaoshuhudia ni
Mkuu wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule (katikati) na Imam
Mkuu wa Msikiti mkuu wa Wilayani Ally Mwabaku.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)