Kampuni
ya mawasiliano ya Vodacom, Tanzania imetoa fursa kwa Watanzania kuweza
kupiga kura na kuchagua mrembo anayevutia zaidi kati ya warembo 30
wanaoshiriki shindano la kumsaka Vodacom Miss Tanzania 2011.
Akizungumza
na waandishi wa habari, Mkuu wa Udhamini wa Vodacom ,George Rwehumbiza,
alisema ili kupiga kura Watanzania watatakiwa kutuma ujumbe mfupi wa
maneno wenye neno MREMBO ukifuatiwa na namba ya mshiriki 'mfano 40' kwenda 15550 ambapo gharama kwa kila ujumbe ni shilingi 150 tu .
Aidha
Rwehumbiza, aliongeza kuwa kila ujumbe mfupi utakaotumwa utampatia
Mtanzania pointi 10 ambapo wateja 20 watakaobahatika kuwa na pointi
nyingi zaidi kila mmoja atajipatia TIKETI mbili za VIP
zitakazomwezesha kwenda kushuhudia fainali ya shindano la Vodacom Miss
Tanzania 2011, itakayofanyika tarehe 10 mwezi septemba katika ukumbi wa
Mlimani city jijini Dares salaam.
Pia
kwa wale watakaohitaji kutoa maoni au mitazamo yao mbalimbali kuhusu
Vodacom Miss Tanzania watapata fursa ya kutuma ujumbe mfupi wa maneno
wenye neno MREMBO ukifuatiwa na maoni kwenda namba 15550.
Akisisitiza
hili Rwehumbiza, alisema ili kuwafahamu warembo wanaoshindania taji la
Vodacom Miss Tanzania 2011, Watanzania wote wanaweza kuangalia kituo
cha Televisheni cha STAR TV leo kuanzia muda wa saa moja jioni pamoja na CLOUDS TV muda wa saa tatu usiku kila siku pia soma magazeti ya Mtanzania, The African, Dimba, Rai na Bingwa.
.
Vodacom kazi ni kwako
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)