Jairo apokelewa kwa kishindo Wizarani, Wafanyakazi wasukuma gari Ngeleja ashangilia kurejea kwake - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Jairo apokelewa kwa kishindo Wizarani, Wafanyakazi wasukuma gari Ngeleja ashangilia kurejea kwake


Wafanyakazi wa Wizara ya Nishati na Madini wakilisukuma gari lililokuwa limembeba Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. David Jairo mara baada ya kuwasili kwenye ofisi za Wizara hiyo.
Wafanyakazi kutoka Idara ya Nishati iliyopo chini ya Wizara ya Nishati na Madini wakilisukuma kwa nyuma gari lililokuwa limembeba Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw David Jairo mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi za Wizara hiyo mapema leo asubuhi.
Wafanyakazi wa Wizara ya Nishati na Madini wakimpokea Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. David Jairo kwa shangwe mara baada ya kuwasili kwenye ofisi za Wizara hiyo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Bw. David Jairo akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa Wizara hiyo mara baada ya kuripoti mapema leo asubuhi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Bw. David Jairo akitafakari jambo mara baada ya kurejea ofisini kwake ili kuendelea na majukumu yake.
Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja akiwa amemkumbatia kwa furaha kama moja ya mapokezi Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. David Jairo mara baada ya kuripoti katika ofisi za Wizara hiyo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari mara baada ya kuripoti ofisini kwake mapema leo asubuhi.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages