Mamlaka ya udhibiti katika sekta ya
nishati na maji (EWURA) imeagiza kampuni kubwa nne za kuuza mafuta ambazo
zimedaiwa kuwa vinara wa mgomo wa kuuza mafuta nchini, kuanza kuuza bidhaa hiyo
mara moja ambapo pia imetoa onyo kali kwa kampuni zinazoendelea na mgomo
huo. Kampuni
zilizotakiwa kurejesha huduma ni BP, Engen, Camel pamoja na Oil Com. Kampuni
hizo pia zimetakiwa kujieleza ndani ya saa 24 kwa nini zisichukuliwe hatua za
kisheria kwa kuvuruga ugavi wa nishati ya mafuta nchini. Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Bw Haruna
Masebu, amesema katika mkutano na waandishi wa habari kuwa kwa mujibu wa sheria
ya uanzishwaji wa EWURA, agizo hilo ni sawa na agizo la Mahakama Kuu ya
Tanzania. “Agizo hilo
pia linawataka kutojihusisha na matendo yeyote ambayo yatavuruga mwenendo wa
ugavi wa mafuta katika soko,” Bw Masebu alisema katika mkutano huo na waandishi
wa habari. Maagizo hayo
ya EWURA yanafuatia mkutano wa wajumbe wa bodi ya wakurugenzi wa mamlaka hiyo
uliofanyika jana jijini Dar es Salaam kujadili hali ya mgomo wa mafuta.
Habari Kwa Hisani Ya John Bukuku - Full Shangwe Blogu
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)