Naibu Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Asha Rose Migiro, akizungumzia umuhimu wa Taifa
kusimamia haki ya mtoto ya kuishi kwa amani na furaha bila kufanyiwa Ukatili wa
aina yoyote, wakati wa Kilele cha uzinduzi wa ripoti ya Utafiti na Mpango wa
Kitaifa wa kushughulikia "Ukatili kwa Watoto" na mpango wa Udhibiti wa
Taifa.
Baadhi ya
Watoto wa Shule za Msingi mbalimbali wakiandamana katika sherehe za uzinduzi wa
ripoti ya Utafiti na Mpango wa Kitaifa wa kushughulikia "Ukatili kwa Watoto" na
mpango wa Udhibiti wa Taifa.
Naibu
Katibu Mkuu wa Umoja wa Taifa Dkt. Asha Rose Migiro na Waziri wa Maendeleo ya
jamii, Jinsia na Watoto Mh. Sophia Simba wakizindua rasmi RIPOTI YA UTAFITI NA
MPANGO WA KITAIFA WA KUSHUGHULIKIA "UKATILI KWA WATOTO" NA MPANGO WA UDHIBITI WA
TAIFA.
Wadau na watu
mbalimbali kutoka taasisi za Kimataifa na Kitaifa wakifuatilia kwa umakini
kilele cha uzinduzi huo.
Mabalozi
wawakilishi wa nchi mbalimbali nchini wakifuatilia uzinduzi wa ripoti hiyo
HOTUBA
Ninayo furaha kubwa sana
kuwa hapa pamoja nanyi leo hii katika tukio hili muhimu na la kihistoria kama
alivyosema Mheshimiwa Sophia Simba.
Lakini nina furaha ya pekee
kuwa miongoni mwenu kwa sababu mimi ni Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa
niliyetokana na nchi hii nzuri.
Kwa Habari Zaidi <<< BOFYA HAPA >>>
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)