Mwili Wa Marehemu Luteni Jenerali Mstaafu Mayunga Wawasili Nchini - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Mwili Wa Marehemu Luteni Jenerali Mstaafu Mayunga Wawasili Nchini

 
Ofisa wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), akifunga mlango wa gari lililobeba jeneza (pichani)lenye mwili wa Luteni Jenerali mstaafu, Silas Mayunga, uliokuwa ukisafirishwa leo kutoka Uwanja wa Ndege wa Jeshi, Ukonga kwenda kuhifadhiwa Hospitali ya Lugalo, Dar es Salaam.
Juliana Mayunga ambaye ni mjane wa Luteni Jenerali mstaafu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), marehemu, Silas Mayunga, akifarijiwa alipokuwa akilia baada ya mwili wa mumewe kuwasili leo kwenye Uwanja wa Ndege za Jeshi, Dar es Salaam.Mayunga alifariki Jumamosi iliyopita akiwa kwenye matibabu nchini India. Mwili wa Luteni Jenerali Mayunga unatarajiwa kuagwa kesho katika Kambi ya Jeshi ya Lugalo na baadaye nyumbani kwake Shariff Shamba, Ilala, Dar es Salaam.
Picha Zote na Mdau Richard Mwaikenda

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages