Mshambuliaji wa Arsenal Robin van Persie amethibitishwa kuwa nahodha mpya wa klabu hiyo.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28
anayechezea pia timu ya taifa ya Uholanzi, amekuwa katika klabu ya
Arsenal tangu mwezi wa Mei mwaka 2004 na anachukua nafasi hiyo kutoka
kwa Cesc Fabregas, aliyehamia klabu ya Barcelona wiki hii. Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amesema: "Van
Persie ni kiongozi kutokana na uchezaji wake, kutokana na ushawishi wake
na ari aliyonayo ya kushinda. "Amekuwa aktika klabu hii kwa muda mrefu na kiufundi ni kiongozi." Van Persie, ambaye msaidizi wake anakuwa mlinzi Thomas Vermaelen, amesema amefurahia kupata nafasi hiyo. "Kuwa nahodha, unakuwa ni balozi kwa klabu na
nipo tayari kwa hilo," amesema Van Persie. "Nimekuwa katika soka kwa
zaidi ya miaka 10, kwa hiyo naelewa namna ya kutekeleza majukumu yangu. "Kila mara unalazimika kuonesha heshima mbele za watu.Van Persie hataiongoza Arsenal katika mechi dhidi ya Udinese usiku wa Jumanne katika kuwania nafasi ya kufuzu mechi za Ubingwa wa Ulaya, kwa sababu anatumikia adhabu ya kufungiwa mechi moja na Uefa.
Lakini atachukua hatamu za kuiongoza Arsenal watakapomenyana na Liverpool katika uwanja wa Emirates siku ya Jumamosi kwenye pambano la Ligi Kuu ya Soka ya England.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)