Kaimu
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Meshak Sadick akisikiliza maelekezo
kutoka kwa Katibu Msaidizi sehemu ya Serikali za Mitaa, Elizabeth Munuo,
ambayo yalielezea jinsi kinyago alichoshika kilivyokuwa kinatumika
katika sherehe za ngoma binti anapokuwa hapo zamani, katika uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika mkoa wa Dar es Salaam uliofanyika jana.
Wanafunzi wa Shule mbalimbali na wananchi wakiangalia mfano wa nyumba katika uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika,uliotengenezwa
na wanafunzi wawili, mmoja wa kidato cha kwanza na mwingine kitado cha
pili wote wa shule ya Sekondari ya Tandika Wilaya ya Temeke Dar es
Salaam. Uzinduzi huo ulifanyika katika uwanja wa Mnazi Mmoja jana.
Wanamuziki
wa Bendi ya Msondo ngoma Hamisi Mnyupe(kushoto),Roman
Mng’ande(katikati) na Eddo Sanga(kulia) wakiwajibika jukwaani katika
uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika mkoa wa Dar es Salaam uliofanyika jana katika viwanja vya Mnazi moja jana.
Kaimu
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Meshak Sadick akisikiliza maelekezo ya
ubora wa thamani za ndani kutoka kwa Mkurugenzi wa Jaffer Ind.Sain Ltd
,Vishal Sing Sain zinazotengenezwa na kampuni hiyo kwa kutumia
Malighafi inayopatikana nchini Tanzania wakati wa Maadhimisho ya miaka
50 ya Uhuru kwa Mkoa wa Dar es Salaam katika Viwanja vya Mnazi Mmoja
jana.
Habari Kwa Hisani Ya Janeth Tabasamu
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)