Nyota wa mchezo wa kikapu nchini Marekani anayechezea timu ya Orlando Magic,Dwight Howard ambaye pia ni mkurugenzi wa taasisi ya D12 Foundation akiwa na mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha na Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa(Kushoto) pamoja na mkewe,Regina Lowassa mara nyota huyo alipotembelea shule ya sekondari ya wasichana ya Kipok iliyopo wilayani Monduli juzi na kutoa msaada wa kiasi cha fedha 90 milioni kwa lengo la kusaidia ujenzi wa mabweni ya wanafuzi shuleni hapo.
Nyota wa mchezo wa kikapu nchini Marekani ambaye pia ni mkurugenzi wa taasisi ya D12 Foundation ya nchini humo ,Dwight Howard Akiwa katika picha ya pamoja na Wanafunzi wa wa shule ya sekondari ya Kipok iliyopo wilaya ya monduli
Nyota wa mchezo wa kikapu nchini Marekani ambaye pia ni mkurugenzi wa taasisi ya D12 Foundation ya nchini humo ,Dwight Howard akimkabidhi hundi ya thamani ya sh,90 milioni mkuu wa shule ya sekondari ya Kipok iliyopo wilayani Monduli,Felister Lukumay kwa lengo la kusaidia ujenzi wa mabweni shuleni hapo jana,katikati anayeshuhudia ni mbunge wa jimbo hilo,Edward Lowasa.
Nyota huyo wa kikapu nchini Marekani anayechezea timu ya Orlando Magic akiwa na watu mbalimbali waliofika katika hafla ya kukabidhi hundi ya kiasi cha sh,90 milioni kwa lengo la kusaidia ujenzi wa mabweni ya wanafunzi shuleni hapo.Picha na mpiga picha wetu
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)