Mimi
leo asubuhi jumapili ya tarehe 20/08/2011, nilikuwa nawasafirsha ndugu
zangu wawili kuelekea mkoa wa Arusha kupitia basi la Dar Epress liliwa
na registration no. T 367 ARH, departure time ya basi ilikuwa ni saa
12:00 asubuhi ambalo
linaondokea pale shekilango au urafiki kama wengi tulivyozoea kupaita,
nilikata tiketi 2 ambayo thamani yake ni shs 25,000/= kwa kila moja,
wakati tunapandisha mizigo kwenye buti ya gari alitokea kijana mmoja na
kusema kwamba unatakiwa kulipia mizigo, kwa utaratibu kabisa
nilimuuliza kwa nini? akasema mizigo hiyo ni mingi, nikamwambia kuwa
huwezi kupima mizigo kwa macho.
mizigo inapimwa na mizani na uniambie ni unzito wa kg ngapi abaria
anapokata basi ndio anapewa free na baada ya kuoneka abaria amezidisha
mizigo basi ndipo mtapiga mahesbu kutokana na kg ambazo zimezidi halafu
alipie, lakini yule kijana alikuja juu sana nakusema haiwezeani
inabidi ulipie ndio kun kaka mmoja akanishauri nimuone supervisor wao
kwa jina ni mzee mosha, nilifuata supervisor na kumuomba twende naye
aone ile mizigo na kwa makubaliano ya kupima ndio naweza kulipia, yule
supervisor alikwenda kuona na kusema kuwa hakuna neno rudisha mizigo
kwenye basi then safari ianze, lakini kondacta wa lile basi ambaye
sikuweza kupata jina lake alitokea na kumwambia yule supervisor kuwa
wewe ni supervisor mpaka kwenye buti na kuotoa maneno ya kashfa sana,
ndipo supervisor akaamuru gari iondoke baada ya mizigo ya abaria wangu
kurudishwa kwenye gari.
Baada
ya basi uondoka niliwasikia dada mmoja na kaka mmoja nao pia
wakilalamika kuwa nao pia wamepata matatizo kama yangu baada yakuambwa
alipipe godoro dogo la mwanafunzi, kwa bahati nzuri wao walikuwa
wanafahamiana na mtoto mwenye kampuni ya mabasi waipigia simu na kufika
pale ndio akaweza kupakia.
Nakumbuka
haya mabasi yalisababisha ajali kipindi fulani hivi na watu waikuwa
wanayaogopa na watu kuwaita chinja chinja, lakini walijitahidi na huduma
nzuri mpaka wananchi wakasahau yale machungu ya ndugu zao ufariki
katika ajalli.
Sasa ombi langu ni kwamba Winzara husika wasimamie jambo hili kwa ni usumbufu kwa wananchi na vipingele vyangu ni kwamba
- Wenye mabasi waandike kwenye ticketi ni kg ngapi ni free?
asanteni
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)