Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikaguwa Gwaride lililoandaliwa maalum kwa
ajili ya kumuaga wakati alipokuwa akiondoka uwanja wa ndege wa Fevereiro uliopo
jijini Luanda, Angola leo Agosti 19, baada ya kumalizika kwa mkutano wa 31 wa Viongozi
wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliomalizika
jana Agosti 18
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini kitabu
cha maafikiano yaliyotokana kuhusu itifaki ya pamoja kwa nchi za SADC inayohusu
udhibiti wa fedha chafu sambamba na katiba ya ushirikiano wa majeshi ya Polisi
kwa nchi wanachama wa SADC yaliyoafikiwa katika mkutano wa 31 wa Viongozi wa Nchi wanachama wa SADC mjini Luanda Angola jana Agosti 18.
Waziri
wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe na Wajumbe kutoka nchi mbalimbali
za Jumuiya ya Maendeleo zilizopo kusini mwa afrika (SADC), wakiwa katika
mkutano wa 31 wa Viongozi wa Jumuiya hiyo uliomalizika nchini Luanda Angola
jana Agosti 18
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisalimiana na Waziri Mkuu wa Zimbabwe, Mogan Changirai, walipokutana kwenye mkutano wa 31 wa Viongozi
wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliomalizika jana
Agosti 18, nchini Luanda Angola. Picha
na Amour Nassor-OMR
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)