Kada wa Chama Cha Mapinduzi-CCM Ndugu PETER KAMFUMU ameongoza kura za maoni zilizopigwa na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora kwa ajili ya kuomba kugombea Ubunge Jimbo la Igunga lililoachwa wazi na Rostam Azizi (pichani)aliyejiuzulu.
Taarifa
iliyotua hivi punde katika mtandao huu kutoka radio Uhuru Fm inadai
kuwa Ndugu KAMFUMU ambaye pia ni Kamishna wa Nishati katika Wizara
ya Nishati na Madini amepata kura 588 kati ya kura 928 zilizopigwa na
Wajumbe wa Mkutano huo katika uchaguzi uliofanyika jana Mjini Igunga.
Katibu wa CCM Wilaya ya Igunga Ndugu NEEMA ADAM ameiambia
Uhuru FM kwa njia ya Simu kuwa jumla ya wanachama wa Chama Cha
Mapinduzi Kumi na Tatu wamepigiwa kura za maoni katika mkutano huo.
Wanachama wengine waliopigiwa kura ni pamoja na Ndugu JAFARI
ALI OMAR kura 163, SHAMSI FEROUZ IBRAHIMU kura 36, Ndugu HAMIS MAPINDA
kura 36, Ndugu NGASA NIKOLAUS kura 18, Ndugu SELF HAMIS kura 13 na
Ndugu SHIRE MASHAURI kura 16. Wengine ni Ndugu HAMAD SAFARI kura 5, Ndugu MKOBA SHABAN kura
5 Ndugu DANIEL MBOJE kura 4, Ndugu ADAM KAMANI kura Tatu na Ndugu
AMINA FUNDIKILA kura Saba.
Kulingana na Katibu huyo wa CCM Wilaya ya Igunga majina hayo
yote yatapelekwa ngazi ya Mkoa ambayo nayo itayapitia na kisha
kuyapeleka katika Kamati Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi kwa
maamuzi zaidi.
Na Francis Godwin
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)