Unaweza kutuambia kidogo kuhusu wewe na blog yako?
Kwanza
kabisa napenda kuchukua nafasi kujitambulisha tena naitwa Josephat
Lukaza. Na mimi ni mwanafunzi wa mwaka wa pili sasa wa Chuo Kikuu Cha
Dodoma. Nafanya shahada ya kwanza ya elimu ya jamii (Sociology).
Nimeanza kublog baada ya kuhitimu masomo yangu ya kidato cha sita mnamo
mwezi wa 3 mwaka 2009. Kutokana na kutokojua labda umuhimu wa blog
sikuweza kuona umuhimu wakuwa na blog hapo mwanzoni lakini baada ya
kuanza masomo yangu katika chuo kikuu ndio nilipoanza kufikiria kitu
ambacho kinaweza kunitofautisha mimi na wengine ndipo hapo nilipoamua
sasa kuanzisha blog nyingine sasa ambayo ndio hii ya LUKAZA ya link http://josephatlukaza.blogspot.com
lakini haya yote niliweza kuyafanya baada ya kuweka umakini na
kuchukulia hii kama sehemu ya kazi yangu na kupenda kujifunza juu ya
blog na maswala mazima ya teknolojia na ndipo nikaanzisha rasmi blogu
hii. Blog hii niliitengeneza mwenyewe mnamo tarehe 18 October 2010
wakati nipo likizo ndefu ya kumaliza mwaka wa kwanza wa masomo na mpaka
sasa ina miezi 9 na siku kadhaa ikienda mwezi wa 10.
Je blog yako unatumia jina lako kamili au
unablog kwa kutumia kivuli kingine na watu wanasoma na kuenjoy blog
yako lakini hawajui wewe ni nani?
Ya blogu yangu mimi
natumia jina langu halisi ambalo ndio jina linalotumika kwenye vyeti na
maswala ya kiofisi..Wadau wanaosoma blogu yangu ni kweli wanasoma na
kuenjoy na mpaka muda mwingine napata maoni na mawazo mengi sana juu ya
kufanya blogu yangu iwe nzuri zaidi.
Ni miaka mingapi sasa umekua ukiblog?
Kwa
kweli nilianza kublog mwezi wa tatu mwaka 2009 lakini sikufuatilia sana
na kuamua kuacha swala zima la kublog. Tarehe 18 October 2010 ndipo
niliporudi tena na kuamua kublog rasmi. Hii yote ni kutokana na maoni
mengi ya rafiki zangu, na courage kutoka kwa watu wangu wa karibu sana
na ndipo nilipoamua kufanya ndio kazi yangu sasa baada ya kuhitimu.
Ni nini kilikufanya uanzishe blog?
Kilichonifanya
nianzishe blogu hii, kwanza ni kwa vile naweza kutengeneza blogs, Hivyo
kwa sababu naweza kutengeneza blogs na hata websites ndipo nilipoamua
kuanzisha blog yangu tena. Pili niliona umuhimu wa kuwa na blog kutokea
kwa watu wengine kama Issa Michuzi na Haki Ngowi hawa jamaa ndio
walionipa moyo zaidi na kuona umuhimu wa kuwa na blog. Mtu kama Issa
nilikua natembelea blogu yake na kuvutiwa sana na blogu yake na ndipo
nilipoaanza kublog. Haki Ngowi aliweza kunipa moyo sana na kunifariji
na kunisaidia pale ambao yeye anaweza kwa namna hiyo nikaamua kublog
kwa kuona kuwa naweza kupata support kutoka kwa Haki Ngowi na wengineo.
Kwa Mahojiano Zaidi <<< BOFYA HAPA >>>
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)