Hivi ndivyo majani yanavyo onekana katika Mbuga ya wanyama Mikumi ambapo imegeuka sehemu ya kuchungia mifugo
Kundi la Mbuzi na Ng'ombe wakiwa wanachungwa kati kati ya Mbuga Mikumi Katika
hali isiyo ya kawaida Kamera yetu ilipata taswira hizi kati kati ya
Hifadhi ya wanyama Taifa Mikumi ambapo watu waliokuwa na kundi na
Ng'ombe na mbuzi walionekana wakichunga eneo hilo, hata hivyo
tulijitahidi kusimama na kuwahoji wahusika ambao walikua na mifugo
hiyo, Hawakuwa na lakusema zaidi ya kudai kuwa Kutokana na uhaba wa
Nyasi ndio maana waliamua Kuchungia mifugo hiyo katika hifadhi hiyo, na
walipo ulizwa juu ya hatari ya wanyama kama Simba walisema kuwa kwa
mchana simba hawakai maeneo ya barabara na ndio maana wanachungia
mifugo hiyo kando kando ya bara bara. Jitahada za kuwasaka wahusika wa
hifadhi hiyo zilifanyika bila mafanikio. Hata hivyo Mwandishi wetu
aliwasihi kuwa ni hatari kuchunga mifugo eneo hilo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)