Rais wa Miss Utalii Tanzania, Gideon Chipungahelo |
Wakati shindano la Miss Utalii Dodoma 2011/2012, limepangwa kufanyika siku ya Idd Mosi , katika ukumbi wa Royal Village Mjini Dodoma, makampuni na watu mbalimbali wamejitokeza kudhamini shindano hilo, litakaloshirikisha warembo 18 kutoka Wilaya zote za Mkoa wa Dodoma.
Kampuni ya Dodoma Innovation and Production Limited wazalishaji na wasambazaji wa Maji ya Kunywa ya ASANTE WATER, wamethibitisha kudhamini shindano hilo kupitia maji hayo ya ASANTE WATER.
Akithibitisha udhamini huo, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Constantine Boehl,alisema kuwa kampuni yake kupitia maji ya Asante Water wanadhani shindano hilo kwa udhamini wenye thamani ya shilingi milioni tano, ukijumuisha fedha taslimu na bidhaa za maji ya Kunywa.
“ Tumeamua kudhamini shindano la Miss Utalii Dodoma 2011/2012, tukiamini kuwa ni moja ya njia ya kusaidia kuutangaza mkoa wa Dodoma kitamaduni, kiuwekezaji na kitalii, pia hii italuwa ni fulsa ya pekee kwetu kutangaza bidhaa zetu zenye hadhi ya kimataifa ambazo tunazalisha hapahapa Dodoma.
Ni fahari na heshima kwetu kuwa sehemu ya wadhamini wa shindano hili linalolenga kutangaza utalii, utamaduni wa Tanzania na mianya ya uwekezaji iliyopo Dodoma, ili kuvutia wawekezaji na watalii kuja Dodoma, ambayo ni makao makuu ya Tanzania “.
Akiwashukuru wadhamini hao,Mkurugenzi wa Miss Utalii Tanzania Mkoa wa Dodoma na Kanda ya Kati Charles Aloyce Gabriel, alisema kuwa anawashuku sana ASANTE WATER kwa udhamini wao na kuahidi kuwa watautumia kwa Malengo yaliyo kusudiwa, pia aliwaomba wafanyabishara, makampuni binafsi na ya umma, kujitokeza kudhamini kudhamini shindano la Miss Utalii Dodoma 2011/2012, ikiwa ni fulsa ya pekee kwao kuunga mkono juhudi za Serikali ya mkoa wa Dodoma ya kuutangaza mkoa huo, pia kwao kujitangaza na kutangaza bidhaa zao kupitia shindano hili .
Washindi wa kwanza hadi wa Tano na wa Vipaji watawakilisha Mkoa wa Dodoma katika fainali za Kanda za Miss Utalii Tanzania kanda ya Kati 2011/2012 zitakazo fanyika mkoani Tabora mwezi Novemba 2011.
Kampuni ya ASANTE WATER inaungana na wadhamini wengine ambao ni pamoja na KIFIMBO FM ya Dodoma, CLOUDS RADIO ya Dar es Salaam, New Dodoma Hotel, Royal Village ya Dodoma, Peter Fashion LTD ya Dodoma na Shabiby Bus Services ya Dodoma. Wadhamini wengine ni pamoja na Auckland Travel & Tours, Image Masters na Dar es Salaam City Collage zote za Dar es Salaam.
Mazoezi kambi ya mazoezi ya warembo hao itaanza siku ya Jumapili tarehe 22 katika hoteli ya New Dodoma Hotel, chini ya Miss Utalii Dar es Salaam 2010/2011 ambaye pia ni Mshindi wa tano wa Taifa Sophia Athumani wakishirikiana na Miss Utalii Vyuo Vikuu kanda ya kati 2010/2012 Tabia Msuta, na Miss Utalii Njombe 2010/2012 Neema Andrew.
Aidha aliwataka warembo wa Dodoma kuendelea kujitokeza kuchukua fomu za kuomba kushiriki, ambazo zina patikana Kifimbo FM Radio, Maisha Club, Maputo Bar, VETA HOTEL, DODOMA HOTEL ,CF Communication Dodoma, Vero Saloon, Marvel Saloon & Boutique na Salome Boutique mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu ni 23 -8-2011.
Imetolewa na:
Charles Aloyce Gabriel
Mkurugenzi Miss Utalii Tanzania Mkoa wa Dodoma na Kanda ya Kati.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)