Mashabiki wa Yanga wakishangilia ushindi huo wa timu yao baada ya kuibika na ushindi wa penati 5-4.
Mashabiki wa Yanga wakishangilia huku wakiwa na bango linalowakebehi watani wao wa Jadi Simba.
Kikosi cha kwanza cha Yanga kulichoanza mtanange wa leo.
Godfrey
Taita wa Yanga (kushoto) akichuana kuwania mpia na Beki wa St. George
ya Ethiopia, Abebaw Butako, wakati wa mchezo wa Fainali za Kombe la
Kagame uliochezwa leo jioni kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam,
ambapo Yanga imefanikiwa kutinga katika hatua ya fainali hizo baada ya
kuwagalagaza St. George kwa mikwaju ya Penati 5-4.
Dakika
90 za mchezo huo zilimalizika kwa timu hizo bila kufungana na hatimaye
kuongezwa dakika 30 ambazo pia zilimalizika bila kupatikana mbabe jambo
lililopelekea timu hizo kuingia kwenye hatua ya kupigiana mikwaju.
Kwa
hatu hiyo sasa Yanga itakutana na watani wake wa Jadi Simba ambao nao
pia jana walifanikiwa kutinga katika fainali hizo kwa njia ya mikwaju ya
penati, St. George sasa itavaana na El-Mereikh ya Sudan katika kusaka
mshindi wa tatu wa michuano hiyo mchezo unaotarajia kupigwa keshokutwa
jumapili mchana kwenye uwanja wa Taifa kabla ya mchezo wa fainali wa
Watani hao wa jadi utakaochezwa siku hiyo hiyo
Picha na Blog ya Michuzi Na Sufiani Mafoto
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)