WADAU WA SERENGETI FIESTA 2011 MBEYA WAFIKA SALAMA NA KUANZA KUKATA MITAA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

WADAU WA SERENGETI FIESTA 2011 MBEYA WAFIKA SALAMA NA KUANZA KUKATA MITAA

Msanii Dizo Busness kushoto na Ispector Haroun nyuma wakishuka kwenye gari mara baada ya kufika katika hoteli ya Mount Livingstone jijini Mbeya, tayari kwa kukamua vilivyo katika mwendelezo wa Msimu wa Dhahabu na Serengeti Fiesta, tamasha linalotarajiwa kufanyika kesho kwenye uwanja wa Sokoine jijini humo. Wasanii hao pamoja na watangazaji na wafanyakazi wengine wameingia jijini Mbeya kwa msafara mkubwa ukitokea Uyole, ambapo mapikipiki zaidi ya 15 yaliupokea msafara huo huku gari la matangazo likipiga matangazo na muziki kuashiria kwamba shughuli ya Serengeti Fiesta ndiyo kwaanza imeanza, na itahitimishwa kesho mkoani humo. Wasanii mbalimbali tayari wamewasili jijini Mbeya kama vile Profesa Jay, 2%, Inpector Haroun, Chid Benz, Rais wa Masharobaro, Godzilla, Jafarai, MwanaFA, Belle9 Juma Nature, Luteni Kalama, Joh Makini na wengine wengi na wako tayari kuwasha moto katika tamasha hilo la Serengeti Fiesta.
Kushoto ni Profesa Jay na Khamis Mandi aka B12 ambaye ni mtangazaji wa Clouds nao wakishuka kwenye gari.
Hapa msafara ndiyo uko Mafiati unakata kona kuelekea mjini.
Mafiati hapa huu ni msafara wenye magari yapatayo kumi ukiwa umebeba wasanii mbalimbali, ikiwa ni pamoja na gari linalotangaza matangazo ya moja kwa moja katika kituo cha Radio Clouds.
Hapa msafara ukiingia ukitokea Uyole nje kidogo ya jiji la Mbeya ukiongozwa na mapikipiki kama unavyoona katika picha hii.
Hapa ni Mafinga kijiji kinachoitwa Kinyanambo tulisimama hapa na kunyoosha kidogo viuongo kulia ni John Kutoka Serengeti Breweriers, Allan Chonjo Meneja wa Kinywaji cha Serengeti Lager na Rubani wetu
Hapa pia tulikuta hii salon inaitwa Chidy Benz kama kibao kinavvosomeka. 
 
Na John Bukuku - Full Shangwe Blogu

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages