Kambi za watu wanaokimbia janga la ukame uliotanda huko Afrika mashariki zimeanza kuchipukia ndani ya nchi ya Somalia, kwa mujibu wa shirika la watabibu la Medecins Sans Frontieres.
Katika kipindi cha siku chache watu waliongezeka ndani ya kambi moja kufikia watu 5,000.
Shirika hilo lina uwezo wa kutoa huduma ya matibabu, lakini haina chakula cha kuweza kuwapa.
Hadi sasa mamiya ya Wasomali wamekuwa wakimiminika kwenye mipaka ya Ethiopia na Kenya, wakiwasili kwenye kambi kabambe ya wakimbizi iliyozidiwa kwa idadi ya watu.
Joe Bellivue wa shirika la Medecins Sans Frontier ameiambia BBC kuwa kuzuka kwa kambi ndani ya Somalia ni tukio jipya na ishara ya jinsi gani watu wanavyohitaji msaada.
Hii kwa kweli ni hali ambayo haijawahi kushuhudiwa ndani ya Somalia kwenyewe.
Bw.Belliveau amesema kuwa kumekuepo na ongezeko la kuwepo kwa kambi katika eneo labonde la Juba.
Takriban juma mja lililopita, idadi ya watu huko ilikuwa karibu ya familia mia tatu. Lakini katika kipindi cha siku chache idadi hiyo imeongezeka hadi familia mia nane,alisema Bw.Belliveau.
Bw.Belliveau alieleza kuwa ishara ya watu kuacha nyumba zao na familia zao na kujiunga kwenye kambi zenye msongamano ni bayana kwamba wameishiwa imani,matumaini na uvumilivu.
Shirika la MSF bado lina shida ya kupewa ruhusa kutoka Al Shabab kusafirisha bidhaa kwa ndege kuingia nchini Somalia pamoja na kuwaleta wataalamu wa huduma za misaada.
Source: BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)