BancABC yadhamini mkutano wa chama cha Wanawake wafanyabiashara Tanzania (Tanzania Women Chamber of Commerce – TWCC) - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

BancABC yadhamini mkutano wa chama cha Wanawake wafanyabiashara Tanzania (Tanzania Women Chamber of Commerce – TWCC)

BancABC Tanzania ambayo ni kampuni tanzu ya Atlas Mara na ambao imeorodhesha  kwenye soko la hisa la London, mwishoni mwa wiki ilidhamini mkutano wa  kila mwezi wa chama cha wanawake wafanyabiashara Tanzania (Tanzania Women Chamber of Commerce TWCC) mkutano ambao uliwaleta pamoja wanachama zaidi ya 250 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar kuzungumzia maendeleo yao na changamoto ambazo wanakubana nazo.

Akiongea wakati wa  mkutano huo, Mkurugenzi wa Kitengo cha Digitali BancABC Tanzania Silas  Matoi alisema kuwa benki ya BancABC inatambua ni umuhimu wa wanawake  kwenye ukuaji wa uchumi wa nchi na ndio sababu benki yake imeweka  mikakati ya kuendelea kuwawezesha na kufikia hatua ya leo ya kuungana na Chama cha Wanawake wafanyabiashara Tanzania (TWCC) kwenye mkutano wake  huu wa kila mwezi.

Matoi alisema kuwa kwenye mkutano huo BancABC imeweza kutambua kuwa wanachama wa TWCC huwa wanashiriki maonyesho  mengi nchini China akitolea mfano kuwa kwa mwezi wa Oktoba na Aprili  mwaka huu, wanachama 150 walishiriki baadhi ya maonyesho ya biashara
nchini China. Hata hivyo, Malai alisema kuwa wakati wa safari zao nchi
China wananchama hao wamekuwa wakikubana na changamoto kadhaa na hasa  linapokuja suala ya kubadilisha fedha na hasa inapotokea dharura.

Ninayo furaha kuwafahamisha ya kuwa BancABC Tanzania inayo suluhiso ya jinsi  ya kupata fedha za kigeni mnapokuwa safarani China. Tunayo kadi ya  malipo ya kabla – YUAN pre-paid Visa card, ambayo itawawezesha kufanya  malipo kwa kwa fedha za China. 


Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa benki ya BancABC Tanzania Upendo Nkini akizungumza na wanachama wa chama hicho wakati wa mkutano wa chama hicho ambao uliwaleta pamoja wanachama zaidi ya 250 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar kuzungumzia jinsi ya kufanya biashara na changamoto wanazokutana nazo. Mkutano huo ulifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na kudhaminiwa na benki ya BancABC Tanzania. 
Mkuu wa Kitengo cha Digitali BancABC Tanzania Silas Matoi akiwazilisha mada wakati wa mkutano wa chama cha Wanawake wafanyabiashara Tanzania (Tanzania Women Chamber of Commerce) ambao uliwaleta pamoja wanachama zaidi ya 250 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar kuzungumzia jinsi ya kufanya biashara na changamoto wanazokutana nazo. Mkutano huo ulifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na kudhaminiwa na benki ya BancABC Tanzania. 

Wafanyakazi wa benki ya BancABC wakimsikiliza kwa makini mmoja wa mwanachama wa chama cha Wanawake wafanyabiashara Tanzania (Tanzania Women Chamber of Commerce) Anna Simbeye wakati wa mkutano wa chama hicho ambao uliwaleta pamoja wanachama zaidi ya 250 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar kuzungumzia jinsi ya kufanya biashara na changamoto wanazokutana nazo. Mkutano huo ulifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na kudhaminiwa na benki ya BancABC Tanzania.
 

Mkuu wa Kitengo cha Digitali BancABC Tanzania Silas Matoi akiwazilisha mada wakati wa mkutano wa chama cha Wanawake wafanyabiashara Tanzania (Tanzania Women Chamber of Commerce) ambao uliwaleta pamoja wanachama zaidi ya 250 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar kuzungumzia jinsi ya kufanya biashara na changamoto wanazokutana nazo. Mkutano huo ulifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na kudhaminiwa na benki ya BancABC Tanzania. 

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages