Waziri
wa Kazi na Ajira Gaudencia Kabaka, akisaini kitabu cha wageni leo
mchana alipotembelea Wizara ya Fedha katika Maadhimisho ya Kimataifa ya
Biashara, Sabasaba jijini Dar es Salaam. Mwingine ni Naibu katibu Mkuu
wa Wizara ya Fedha, Elizabeth Nyambibo.
Waziri
wa Kazi na Ajira Gaudencia Kabaka akisikiliza kwa makini maelezo ya
mradi wa ujenzi wa nyumba za bei nafuu kutoka kwa Mkurugenzi wa
uendeshaji Patrick Mongella jana jijini Dar es salaam. Nyumba hizo
zinajegwa na Mfuko wa Pensheni kwa watumishi wa umma. Waziri huyo na
Naibu Wake Dkt Makongoro Mahanga walipata maelezo ya mradi huo wakati
walipotembelea banda la Wizara ya Fedha katika maonyesho ya 35 ya
kimataifa ya Dar es salaam.
Meneja
wa Mahusiano na Huduma kwa Wateja, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF),
Eunice Chilume, akitoa maelekezo kwa Waziri wa Kazi na Ajira Gaudensia
Kabaka, kuhusu huduma za Matibabu zinazotolewa kwa Wanachama wa
Mfuko huo kwenye Maonesho ya 35 ya Kimataifa ya Biashara wakati waziri
huyo alipotembelea jengo la NSSF mapema leo.
Naibu
Katibu wa Wizara ya Fedha, Elizabeth Nyambibo, akijadiliana na Msemaji
wa Wizara hiyo, Ingahedi Mduma, leo mchana wakati Katibu Mkuu huyo
alipotembelea Wizara ya Fedha kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Biashara,
Sabasaba.Picha zote na Mdau Victor Makinda
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)