Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Robin Goetzsche (kulia)
akishuhudia Mwenyekiti wa Bodi ya Mradi Maji Safi kwa Afya Bora Ifakara
(MSABI), Dk. Honorathy Urassa akitia saini mkataba wa makubaliano
ambapo TBL, imeupatia mradi wa MSABI msaada wa sh. milioni 34.5 za
kusaidia awamu ya pili ya mradi huo.Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa
wiki jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni y Bia Tanzania (TBL), Robin Goetzsche (katikati)
na Mshauri wa Miradi Maalumu wa kampuni hiyo, Phocus Lasway (kulia),
wakitia saini mkataba wa makubaliano na Mradi wa Maji Safi na Afya Bora
Ifakara (MSABI),ambapo TBL imeupatia Mradi huo msaada wa sh. milioni
34.5 za kusaidia awamu ya pili ya Mradi huo. Anayeshuhudia hafla hiyo
iliyofanyika, Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki ni Mwenyekiti wa Bodi ya
MSABI, Dk. Honorothy Urassa.
Mhandisi
wa Mradi wa Maji Safi na Afya Bora Ifakara (MSABI),Naomi Mg'endo
(kulia) akitoa shukrani kwa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Dar es Salaam
juzi, ambayo imeupatia mradi huo msaada wa sh. milioni 34.5 za
kusaidia awamu ya pili ya mradi huo utakaovinufaisha vijiji 20 na watu
wapatao 8000 katika wilaya za Ulanga na Kilombero mkoani Morogoro.
Kutoka kushoto ni Meneja Miradi Maalum wa TBL, Emma Oriyo,Mwenyekiti wa
Bodi ya MSABI, Dk. Honorathy Urassa, Mkurugenzi Mtendaji wa TBL, Robin
Goetzsche na Mshauri wa Miradi Maalumu wa kampuni hiyo, Phocus Lasway.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni y Bia Tanzania (TBL), Robin Goetzsche (kulia)
akimkabidhi Mwenyekiti wa Bodi ya Mradi wa Maji Safi kwa Afya Bora
Ifakara (MSABI), Dk. Honorathy Urassa (kushoto), mfano wa hundi yenye
thamani ya sh. milioni 34.5 za kusaidia awamu ya pili ya mradi huo.
Wanaoshuhudia makabidhiano hayo yaliyofanyika Dar es Salaam, mwishoni
mwa wiki ni; Mshauri wa Miradi MaaluMU wa TBL, Phocus Lasway (wa pili
kulia) na Mhandisi wa MSABI, Naomi Mg'endo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)