EL-MEREIKH MSHINDI WA TATU KAGAME CUP, YAICHAPA ST. GEORGE 2-0 - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

EL-MEREIKH MSHINDI WA TATU KAGAME CUP, YAICHAPA ST. GEORGE 2-0

 Hadi mwisho wa mchezo wa kuwania nafasi ya tatu katika fainali ya kombe la Kagame, ubao wa matangazo ulikuwa ukisomeka kama hivi.
Beki wa El-Mereikh ya Sudan, (kushoto) akimdhibiti mshambuliaji wa St. George, wakati wa mchezo wa kuwania nafasi ya tatu Kombe la Kagame uliomalizika hivi punde katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo El-Mereikh wameibuka na ushindi wa mabao 2-0, ambapo mabao yote yamepatikana kipindi cha pili cha mchezo huo. Mchezo wa fainali hiyo baina ya Yanga na Simba zote za Dar unakaribia kuanza ambapo tayari timu zote zimekwishaingia uwanjani zikiwa zinapasha misuri kuwa na ukurasa huu hadi mwisho utakaokuwa ukikuletea yanayojiri uwanjani hapa.
Na Sufiani Mafoto

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages