VODACOM TANZANIA YAING'ARISHA ZANZIBAR MUSIC AWARDS - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

VODACOM TANZANIA YAING'ARISHA ZANZIBAR MUSIC AWARDS

 Meneja wa Vodacom  Tanzania kanda ya Zanzibar Mohamed Mansour kulia akimkabidhi Tunzo Mwanamziki bora wa kiume wa nyimbo za kizazi kipya Juma Twenty kwenye Zanzibar Music Award,zilizofanyika juzi mjini Zanzibar na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.
 .Mwanamziki wa kizazi kipya Baby J akiwa ameshikilia Tunzo yake aliyejinyakulia kwenye Zanzibar Music Award 2011, kuwa  mwanamziki bora wa kike wa muziki wa kizazi kipya ,zilizofanyika  juzi mjini Zanzibar na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania,kulia ni Hagai Samson aliyemkabidhi tunzo hiyo.
Mbunge wa Jimbo la Uzini Zanzibar na Mkurugenzi wa Zanzibar Media Corporation Seif Khatibu kulia akiwa kwenye picha ya pamoja na mshindi  bora wa kike wa nyimbo za asilia Sada Mohamed mara baada ya kumkabidhi tunzo yake kwenye Zanzibar Music Award,zilizofanyika juzi mjini Zanzibar na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.
 .Mjumbe wa NEC Aisha Kigoda kulia akimkabidhi Tunzo msani bora chipukizi wa kike  Sauna G kwenye Zanzibar Music Award,zilizofanyika juzi mjini Zanzibar na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.
 Aaah tamaduni zetu za mwambao hatuziachi kata kidogo kwenye Zanzibar Music Award tunaburudisha.
 Baadhi ya masharobaroz walioudhuria Zanzibar music award.
 Mwanamziki wa kizazi kipya Baby J akionysha Tunzo yake ya pili mara baada ya kukabidhiwa na Meneja wa Zenj Fm.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages