Mwenyekiti wa CCM Singida vijijini, Narumba Hanje
akisoma Agano jipya kitabu cha Wagalatia mbele ya mkutano mkuu wa UVCCM
Singida vijijini juzi.
Kushoto ni katibu wa UVCCM Singida vijijini Rubein
na anayefuata ni mwenyekiti wa jumui ya ya wazazi Singida vijijini,
Elia Digha.
Baadhi ya wajumbe wa mkutano mkuu wa UVCCM Singida
vijijini.Picha zote na Nathaniel Limu
---
Na Nathaniel Limu-Singida.
Mwenyekiti wa CCM Singida vijijini Narumba Hanje,
amekitabiria Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kwamba
hakitaingia Ikulu milele kwa madai kuwa kimepoteza mwelekeo baada ya
kuanza kutumia mbinu chafu ambazo hazitawasaidia kufikia lengo lao.
Hanje ametoa utabiri huo
wakati akifungua mkutano mkuu wa Jumuiya ya umoja wa vijana (UVCCM)
uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa shirika la Pride Singida Mjini.
Alisema CHADEMA sasa kimeacha
kuwaeleza wananchi kitawafanyia nini ili waweze kuleta maendeleo
endelevu, na badala yaje kueneza fitina, hasira, uadui, uzushi.
Aidha, Hanje amedai
kuwa Chama hicho kimeundwa, ‘kiundugunaizesheni’ na kwamba hakina
demokrasi na kuwa na mwonekano wa taasisi binafsi, na kuongeza kuwa
kimepoteza muda mwingi kwa kuzunguka na kufanya maandamano ambayo
hayana tija kwa wananchi.
Mwenyekiti huyo amedai chama hicho kimeonyesha dhahiri kwamba
hakiwatakii mema Watanzania baada ya kuanza kuwadanganya na kuwashawishi
wasichangie maendeleo kwa madai kwamba jukumu la kuleta maendeleo ni
la serikali pekee.
“Sisi hapa mjini,
tunachangia mambo mengi hata ya uzoaji wa takataka, sembuse maendeleo”,
alihoji na kuongeza “CHADEMA hawana ubavu tena wa kuchukua nchi,
wamepoteza mwelekeo, wamefikia mahali wanaifananisha Tanznaia na Misri”.
Hanje alisema
CHADEMA ni ya kuogopwa kama ukoma, kwa madai kwamba viongozi wa chama
hicho,wanatumia nafasi zao kujaza watu wa ukoo wao katika nafasi mbali
mbali za uongozi.
Katika
kuujengea nguvu utabiri wake huo, mwenyekiti huyo alisoma Agano jipya
kitabu cha Wagalatia 5 mstari mdogo kuanzia 19-21.
Pamoja na mambo
mengine, mistari hyo inasema ‘Fitina, wivu, hasira, husuda na mambo
yanayofanana na hayo, katika hayo, nawaambia kwamba watu watendao mambo
ya jinsi hiyo, hawataurithi ufalme wa Mungu.’
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)