TANZANIA KUPATA TUZO KATIKA KILELE CHA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

TANZANIA KUPATA TUZO KATIKA KILELE CHA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Hawa Ghasia akipata maelezo kutoka kwa Afisa Maendeleo ya Jamii Mwandamizi  wa Wizara ya Fedha William Gabriel Ghumpi   jana jijini Dar es salaam wakati Waziri huyo alipotembelea banda la Wizar hiyo.Picha na Tiganya Vincent-MAELEZO.
--
Na Magreth Kinabo-MAELEZO


Imeelezwa kuwa Tanzania ni nchi mojawapo itakayopata tuzo ya kimataifa ya utoaji wa huduma  ya daraja la kwanza katika  sekta ya umma kupitia Mpango wa Kurasimisha Rasilimali za  za Biashara  za  Wanyonge (MKURABITA) katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Utumishi wa Umma ya Umoja wa Mataifa(UN)na Barani Afrika.     Tuzo hiyo itatolewa kwa Tanzania  na UN baada ya kufanya vizuri katika mpango  huo wa kwenye kilele cha maadhimisho hayo ,Juni 23 ,mwaka huu.

Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa  Maendeleo ya Sera kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti na Utumishi wa Umma, Mathias Kabunduguru wakati mkutano wa waandishi wa habari ulioshirikisha baadhi ya viongozi kutoka UN, uliofanyika leo  kwenye ukumbi wa mikutano wa Mlimani City. Nchi nyingine zikazopewa tuzo hiyo  katika kundi hilo kupitia taasisi, mbalimbali, ni Brazil, Canada, Colombia, Misri , India, Mexico, Oman, Poland,  Ureno , Jamhuri ya  Korea, Slovakia, Afrika Kusini na  Thailand. 

    
Aidha Kabunduguru alisema mkutano wa kimataifa wa Utumishi wa Umma utakoambatana na kongamano unafunguliwa kesho  na mgeni rasmi ambaye anatarajiwa kuwa  Waziri Mkuu,Mizengo Pinda, wakati  siku ya kilele mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete.

Alisema  pia kutakuwepo na warsha  za mada  ya utaoaji wa huduma katika sekta ya umma namna  ya kujenga uwezo  wa utumishi wa umma katika siku zinazofatia.      Akizungumzia kuhusu maonyesho yanayoendelea kwenye viwanja vya Mnazimmoja ,  alisema siku ya kilele mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein.Kwa upande wake Mratibu wa mkutano huo kutoka UN, Adrean Albert alisema mpango huo utawawezesha Watanzania kutumia rasilimali  ya ardhi kama mtaji kwa ajili ya kuboresha maisha yao kiuchumi na kijamii.Aliongeza kuwa nchi nyingine zinaweza kujifunza kupitia mpango huo.a ya Fedha ikiwa ni siku ya nne ya maadhimisho ya wiki ya utumishi wa umma.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages