Mashabiki wa timu ya Yanga ya Dar es Salaam, wakishangilia
jukwaani baada ya Yanga kuandika bao la pili katika kipindi cha kwanza,
lililofungwa na Asamoh, baada ya krosi safi kutoka kwa Kigi Makasi, na
kufanya timu hizo kwenda mapumziko Yanga ikiwa mbele kwa mabao 2-1.
Kipindi cha pili Wasudani waliweza kupata bao lililozua utata baada ya
kugonga mwamba wa juu na kisha kurudi uwanjani na kudakwa na mlinda
mlango wa Yanga, huku Mwamuzi wa mchezo huo akiashiria kuendelea kwa
mchezo ambaye alitofautiana na mshika kibendera wake aliyeonysha kuwa ni
goli na kumfanya mwamuzi kuwa na maamuzi mawili, huku akinyoosha mikono
kuashiria kuendelea kwa kipute na wakati huo huo akipuliza kipenga cha
kuonyesha kati kuashiria goli.
Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Godfrey Bony, akiwa jukwaani
na mashabiki wa Yanga akifuatilia kipute hicho, kutokana na kutokuwa
kabisha katika risti ya Timbe.
Raha ya mechi Bao bwana!!!, hapa ni Mhariri wa Gazeti la
Champion, Elius Kambili, ambaye pia ni shabiki wa Yanga, akishangilia
na kuonyesha alama ya 2, baada ya Yanga kufunga bao la pili.
Mashabiki wa Soka wakikata tiketi na kupanga foleni ili
kuingia ndani ya uwanja kushuhudia kipute hicho. Katika mchezo wa leo
watu walikuwa wengi tofauti na jana kiasi kwamba wengine walikosa tiketi
walizokusudia kununua baada ya tiketi ya Sh. 2000 kuuzwa kwa Sh. 6000
na nyinginezo kupandishwa bei baada tu ya mpira kuanza.
Kipute kinaendelea uwanjani.......ilikuwa ni kipindi cha
kwanza.
Source: Sufiani Mafoto
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)