|
Haaa haaaa
ka Mfalme Mswati vile..! Shaggy akiondoka viwanjani hapo huku akinesa
nesa kiaina,wakati huo huo akisindikizwa na vimwana mara baada ya hafla
hiyo fupi ya kusimikwa kufikia kileleni. |
|
Mwanamuziki
Shaggy akionekana mwenye furaha,huku akishangilia mara baada ya
kusimikwa ubalozi wa kabila la Kisukuma,na baadhi ya wazee wa kabila
hilo,ambapo leo walikuwa wakisherehekea siku yao ya mavuno (Bulabo)
ambayo imeanza leo tarehe 26 juni na itakoma julai 3,katika viwanja
hivyo vilivyo maeneo ya Kisesa jijini Mwanza. |
|
Mwenyekiti wa Bodi ya
SBL,Mzee Jaji Mark Boman akizungumza machache mara baada ya mwanamuziki
Shaggy kusimikwa ubalozi wa Kabila la Kisukuma na Wazee maarufu wa
kabila hilo. |
|
Chifu Charles Kaphipa
akizungumza katika tamasha hilo la Bulabo kabla ya kumtawaza
mwanamuziki Shaggy kuwa balozi wa kabila hilo, wanaosikiliza kutoka
kulia ni Chifu Makwaiya, Meneja wa Serengeti Allan Chonjo, Mkurugenzi wa
Masoko (SBL) Caroline Ndungu,Mwanamuziki Shaggy pamoja na Mwenyekiti wa
Bodi ya SBL,Jaji Mark Bomani. |
|
Mwenyekiti
wa Bodi ya SBL,Mzee jaji Mark Bomani akiteta jambo na Mwanamuziki
Shaggy. |
Mwanamuziki Shaggy akiwaimbia moja ya wimbo
wake mbele ya baadhi ya watu waliofika kwenye hafla hiyo fupi ya
kushuhudia kusimikwa Ubalozi kwa mwanamuziki huyo.
|
wacha wee
palinoga ile mbaya .! Wageni wakiwasili huku wakipokelewa kwa heshima na
adabu. |
|
Shaggy
akipata maelezo mafupi kutoka kwa Mzee Pius Ng'wangu wakati alipofika
hapo katika makumbusho ya Bujora. |
|
Pichani kushoto
ni Padre Fabian Mhoja akimkaribisha Mwanamuziki Shaggy ndani ya kijiji
cha makumbusho ya Wasukuma,alipokwenda kutembelea na kujionea mambo
mbalimbali ya tamaduni ya kabila la Kisukuma,Wa pili kushoto ni Meneja
wa kinywaji cha Serengeti Allan Chonjo,Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni ya
SBL,Jaji Mark Bomani,Mkurugenzi wa Masoko wa SBL Caroline Ndugu pamoja
na Meneja Matukio wa SBL Bahati Singh. |
|
Mwanamuziki
Shaggy akisindikizwa na vimwana mara alipowasili kwenye uwanja ambao
sherehe za Kisukuma 'Bulabo'zilipokuwa zikifanyika. |
|
Shaggy akifanunua
jambo mbele ya waandishi wa habari,kulia ni Mkurugenzi wa Masoko wa
kampuni ya Serengeti Breweries Ltd Caroline Ndugu,na kushoto ni Meneja
mawasiliano ya ndani ya SBL,Iman Lwinga pamoja na Meneja wa kinywaji cha
Primeum Serengeti Lager Allan Chonjo. |
|
Mwanamuziki Nguli
kutoka nchini Marekani,Shaggya akiwa na wenyeji wake (Wadhamini) kutoka
kamouni ya Bia ya Serengeti (SBL), alipokuwa akizungumza na baadhi ya
vyombo vya habari mbalimbali,kwenye mkutano uliofanyika mchana katika
hoteli ya Malaika iliopo nje kidogo ya jiji la Mwanza |
Habari kwa hisani ya Jiachie Blog
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)