HALMASHAURI IRAMBA YANUNUA BOTI IENDAYO KASI KUDHIBITI UVUVI HARAMU ZIWA KITANGIRI. - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

HALMASHAURI IRAMBA YANUNUA BOTI IENDAYO KASI KUDHIBITI UVUVI HARAMU ZIWA KITANGIRI.


Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Iramba Mkoani Singida Fortunatus Fwema akizungumzia ujio wa boti hiyo kwenye Kikao cha Kwaida cha baraza la madiwani kilichofanyika mjini Kiomboi-Iramba.
Makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Iramba mkoani Singida Bi.Monica Samweli akiwasilisha utekelezaji wa miradi mbalimbali katika kipindi cha Julai mwaka jana na Machi mwaka huu mbele ya kikao cha baraza la madiwani lililokutana mjini Kiomboi-Iramba.
Madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Iramba wakifuatilia kwa umakini makabrasha yao, kuhusiana na utekelezaji wa miradi mbalimbali kati ya Julai mwaka jana na Machi mwaka huu.Picha na Hillary Shoo
--
Na.Hillary Shoo, IRAMBA.
Halmashauri ya wilaya ya Iramba Mkoani Singida imetumia zaidi ya Shilingi milioni 17.3 kununua boti kwa ajili ya kuthibiti uvuvi haramu kwenye ziwa Kitangiri, wilayani humo.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Fortunats Fwema  kwenye kikao cha kawaida cha baraza la Madiwnai kilichofanyika ukumbi wa halamashauri hiyo mjini Kiomboi.
Fwema amesema kuwa boti hiyo itasaidia pia kudhibiti mapato mengi yanayopotea kutokana na mavuno ya samaki unaofanywa na baadhi ya wavuvi wasiokuwa waaaminifu.


“Kabla ya kufikia uamuzi huu, tulilazimika kulifunga kwanza ziwa, kuanzia Disemba mwaka jana hadi machi mwaka huu,kuwafanya samaki wakue na kuzaliana…..boti hii iendayo kasi itasaidia kudhibiti mapato na uvuvi haramu,”alisema.


Hata hivyo Mkurugenzi huyo amesema kuwa uongozi wa halmashauri kupitia vikao vyake vya ushauri unaandaa taratibu maalumu zitakazowezesha boti hiyo kufanya kazi zake vizuri ili kuleta tija kwenye ziwa hilo.


Halikadhalika Fwema amesema kuwa,mgogoro uliokuwepo katika ziwa hilo na wenzao wa Shinyanga sasa umekwisha baada ya kubainika lipo Iramba kutokana na  ramani ya wizara ya TAMISEMI inavyoonyesha.


Aliyasema hayo  akijibu swali lililoulizwa na Diwani wa kata ya Tulya Luther Mkoma  aliyetaka kufahamu mpango uliopo kuweza kudhibiti uvuvi haramu ikiwemo matumizi ya nyavu ndogo hali inayopoteza mapato mengi.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages