ZIARA YA SPIKA WA BUNGE ANNA MAKINDA WILAYANI MWANGA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

ZIARA YA SPIKA WA BUNGE ANNA MAKINDA WILAYANI MWANGA


 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda akipanda mti wa kumbukumbu katika viwanja vya shule ya sekondari ya wasichana  ya Mtakatifu Theresia wa Avila iliyoko katika wilaya ya  Mwanga mkoani Kilimanjaro jana. Hii ni shule ya kwanza ya wasichana katika wilaya hii.  Aliyeshikilia mti huo ni Mkuu wa Wilaya ya Mwanga Mhe. Athman Mdoe. Shule iko chini ya usimamizi wa jimbo Katoliki la Same na inaongozwa na Masista wa Shirika la Grail Tanzania. Sekondari hii yenye wanafunzi 316 na waalimu 16 inaongozwa kwa tunu kuu tano za maadili na kujitambua ambazo ni kujibu maswali yafuatayo: Mimi ni nani? Niko wapi? Nimekuja kufanya nini? Kwa nini ninasoma? na Niko na nani? (kwa maana ya marafiki).
 Baada ya upandaji wa mti huo, Spika Makinda aliukabidhi kwa mwanafunzi wa kidato cha kwanza, Veronica Bwana, autunze na wakati huo huo kuzungumza na wazazi wa walezi wa wanafunzi kuhusu umuhimu wa kuwasomesha watoto wa kike na umhuhimu wa kuilinda amani ya Tanzania. Pia aliwataka watanzania wote kushiriki katika mchakato mzima wa kuundwa kwa katiba mpya ya Tanzania.
 Kutoka kulia Spika wa Bunge Mhe. Anne  Makinda, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (CCM) Mhe. Abdulrahman Kinana, Mkuu wa Wilaya ya Mwanga Mhe. Athuman Mdoe na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini Mhe. Raymond wakiwa miongoni mwa maelfu ya wananchi walioshiriki katika mazishi ya aliyewahi kuwa Mbunge wa Arusha Mjini (1980-1985) marehemu Hubert Mbaga aliyefariki Aprili 27 na kuzikwa jana nyumbni kwake Usangi.
 Akitoa salamu za rambirambi katikati msiba huo, Spika Makinda aliwataka watanzania kuienzi amani ya taifa la Tanzania kama alivyofanya marehemu Mbaga wakati wa uhai wake kwani alimfahamu vizuri kwa kufanyakazi naye kwa karibu. Picha ndogo ni ya marehemu Hubert Mbaga.
Spika Makinda akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Mzee Hubert Mbaga. Picha na Prosper Minja-Bunge

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages