Na Erasto Stanslaus
KIUNGO mshambuliaji, Haruna Moshi ‘Boban’ (pichani) ametua rasmi Simba baada ya timu yake ya Gefle IF ya Sweden kufanya mazungumzo na kukubali arejee Msimbazi.
Wakala wa Boban, Damas Ndumbaro ‘Shashi’ amefanya mazungumzo na Gefle IF na kuiunganisha Simba ambayo imefanikiwa kumrejesha tena katika klabu hiyo kwa miaka miwili.
Tayari Ndumbaro kwa niaba ya Gefle IF, amesaini mkataba wa kumruhusu Boban kuichezea Simba baada ya kufanya mazungumzo na uongozi wa klabu hiyo ulioongozwa na Makamu Mwenyekiti, Geofrey Nyange ‘Kaburu’.
“Kila kitu kimeenda vizuri na Simba wametoa baadhi ya fedha ambazo wanatakiwa kulipa Gefle na zilizobaki watamalizia kwa awamu mbili. Hivyo kinachotakiwa ni wao kumalizana na Boban ili atue rasmi Simba,” alisema Ndumbaro.
Wakati wakala huyo anasema hayo, Kaburu amesema wameshamalizana na Boban ambaye tayari watani wao Yanga walianza kutaka kumnasa kwa kufanya mazungumzo na Ndumbaro.
“Tulianza kumalizana na Ndumbaro ambaye ni mwakilishi wa Gefle, baada ya hapo tumekutana na kumalizana na Boban na kesho (leo) anatakiwa kuanza mazoezi na wenzake.
“Boban kwa sasa ni mchezaji wa Simba, maana yake amerudi nyumbani,” alisema Kaburu jana wakati akifanya mahojiano na Championi Jumatatu.
Boban alijiunga na Gefle IF akitokea Simba lakini kabla hata hajamaliza msimu alivunja mkataba na kurudi nchini. Lakini akabaki bila timu baada ya Gefle IF kutaka kurudishiwa kitita cha dola 50,000 (zaidi ya Sh milioni 70) ilizolipa kwa Simba

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)