SIMBA WAFANYA MKUTANO MKUU DAR - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

SIMBA WAFANYA MKUTANO MKUU DAR

Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage, akiongea na wanachama.
Timu ya soka ya Simba ya jijini Dar es Salaam leo imefanya mkutano wake mkuu katika ukumbi wa  Bwalo la Polisi uliopo Oysterbay jijini hapa.

Mkutano huo ambao ni wa kwanza tangu viongozi wa timu hiyo waingie madarakani ulikuwa na ajenda tatu: Marekebisho ya Katiba, Taarifa za Fedha na Taarifa ya Kamati ya Utendaji.

Kinyume na wengi walivyokuwa wakifikiria, mkutano huo ulimalizika kwa usalama na wanachama wa timu hiyo waliupongeza uongozi mara baada ya mkutano huo kumalizika.  
Baadhi ya wanachama wa Simba wakiwa mkutanoni
 
Kocha mpya wa Simba, Moses Basena,  raia wa  Uganda akiongea jambo katika  mkutano huo.
 
Rage (kushoto) akiwa na Makamu wake, Geoffrey Nyange (Kaburu) wakifurahia jambo.
 
Wanachama wakiupongeza uongozi baada ya kumaliza mkutano huo kwa amani.
 
Baadhi ya wanachama  wa Simba wakipata msosi.
 
Makamu Mwenyekiti, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ (kulia) akipata msosi na kocha mkuu wa timu hiyo.

(PICHA ZOTE NA ISSA MNALLY)

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages