MSIBA CHUO KIKUU CHA DODOMA NA BUGABO - BUKOBA KAGERA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MSIBA CHUO KIKUU CHA DODOMA NA BUGABO - BUKOBA KAGERA

 Mmoja Wa Wanafunzi Akiwa Amebeba Msalaba Wakati Mwili Ukiwa unapelekwa Katika Gari Kwaajili Ya Kuusafirisha Kwao Bugabo, Bukoba Mkoani Kagera

 Wanafunzi Wakiwa Katika Foleni Kwa ajili Ya Kutoa Heshima Ya Mwisho Katika Ukumbi Wa Chimwaga Uliopo Chuo Kikuu Cha Dodoma
 Wanafunzi Wakipita Kwaajili Ya Kutoa Heshima Ya Mwisho Kwa Mwili Wa Marehemu Thereza Protas
 Wanafunzi Wakisubiri Mwili Wa Marehemu Thereza Protas Uingizwe Kwenye Gari Kwaajili Ya Kuusafirisha Kwao Bugabo Bukoba Mkoani Kagera Kwa mazishi.
Mwanafunzi Wa Mwaka Wa Kwanza THEREZA PROTAS amefariki Dunia Mnamo Tarehe 5/5/2011 majira ya Saa kumi Jioni Katika Hospitali Ya Mkoa Wa Dodoma Mara baada ya Kufikishwa Hapo Kutoka Katika Hospitali Ya Chuo Kikuu Cha Dodoma. Marehemu Alifariki Baada ya Kupungukia Damu Wakati Akiwa na Ujauzito. Mara Baada Ya Wanafunzi Kufika Katika Hospitali Ya Mkoa Wa Dodoma Kujitolea Damu Kwa Bahati Marehemu Alipoteza Maisha.

Mwili Wa Marehemu Umeagwa Katika Ukumbi Wa Chimwaga Jioni Hii Na Kusafirishwa Kuelekea Bugabo Bukoba Mkoani Kagera Kwa ajili Ya Mazishi.

Bwana Alitoa Na Bwana Ametwaa Jina La Bwana Libarikiwe.
Mungu Ailaze Roho Ya Marehemu Mahala Pema Peponi Amina.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages