Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba, baada ya kuweka jiwe la Msingi katika Ofisi ya CCM Tawil la Mtambile leo Mei 16. Dkt. Bilal, yupo katika ziara ya kukagua miradi ya Maendeleo katika mikoa ya Kusini na Kaskazini Pemba.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akifunua kitambaa ikiwa ni ishara ya kuweka jiwe la Msingi katika Ofisi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya Tawi la Mtambile iliyopo Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba leo Mei 16, wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua miradi ya Maendeleo katika Mikoa ya Kusini na Kaskazini Pemba.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akifurahia jambo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd, wakati wa mapokezi ya Makamu wa rais aliyewasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Pemba leo Mei 16, kwa ajili ya ziara yake katika mikoa ya Kusini na Kaskazini- Pemba, kukagua miradi ya Maendeleo . Picha na Muhidin Sufiani-Ofisi ya Makamu wa Rais
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)