FREEMAN MBOWE, ZITTO KABWE NA RAISI KIKWETE WAHUDHURIA MAZISHI YA MAMA MZAZI ANNE MAKINDA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

FREEMAN MBOWE, ZITTO KABWE NA RAISI KIKWETE WAHUDHURIA MAZISHI YA MAMA MZAZI ANNE MAKINDA


 Mwenyekiti wa Chadema Taifa Freeman Mbowe ambaye alifika katika msiba wa mama mzazi wa Spika Anne Makinda jana kijiji cha Yakobi Njombe  kuwakilisha  kambi  ya upinzani bungeni akitoa  salam za kambi ya  upinzani na chama chake katika msiba  huo jana
 Msemaji mkuu wa kambi ya upinzani bungeni Freeman  Mbowe ambaye ni mwenyekiti wa Taifa  wa Chadema akiweka shada la maua katika kaburi la mama mzazi  wa spika wa  bunge Anne Makinda marehemu Tulakela Semnyuha aliyezikwa jana kijijini kwake Yakobi Njombe
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha maombolezo kabla ya kuongoza maelfu ya waombolezaji katika mazishi ya mama wa Spika wa Bunge, Bibi Tulakela Samnyuha, nyumbani kwake Yakobi, mkoani Njombe jana jioni.
 Rais Jakaya Kikwete akichota mchanga tayari kwa kuuweka katika kaburi la marehemu Mama Tulakela Samnyuha, mama wa Spika wa Bunge, Anne Makinda wakati wa maziko ya mama huyo katika Kijiji cha Yakobi, wilayani Njombe mkoani Iringa. Katikati ni mke wa Rais, Mama Salma Kikwete
 Spika Makinda akiweka shada la maua kwenye kaburi la mama yake jana.
 Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashilila akiweka udongo katika kaburi la marahemu.
 Spika Makinda akiwashukuru waombolezaji waliofurika kijijini Yakobi, jana.
 utoka kulia ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Rais Kikwete, Spika Makinda na Mama Salma Kikwete wakijadili jambo wakati wa mazishi ya mama yake Spika Makinda jana jioni.
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda akijadili jambo na Kingozi wa Upinzani Bungeni Mhe. Freeman Mbowe mara baada ya mazishi ya mama mzazi wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yaliyofanyika katika Kijiji cha Yakobi mkoani Njombe jana jioni.
Naibu katibu mkuu wa Chadema Taifa Zitto Kabwe (kulia) akiteta jambo na katibu mkuu wa CCM Taifa Wilson MKama jana   wakati  wakisubiri Rais Jakaya Kikwete kuwasili kijiji cha Yakobi Njombe kwa ajili ya  kuwawakilisha  watanzania katika mazishi ya mama mzazi wa spika Anne Makinda. Picha NA Francis Godwin na Prosper Minja-Bunge, Yakobi-Njombe

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages