Wanafunzi Wa Kitivo Cha Sayansi Ya Jamii, Sanaa na Lugha Wakiwa katika foleni Katika Kituo Cha Kupigia Kura kwaajili ya kuwapigia kura viongozi wanaowania Nafasi za Uongozi Chuo Hapa.
Wanafunzi Wa Kitivo Cha Sayansi Ya Jamii, Sanaa na Lugha Wakiwa kwenye Foleni Tayari kwa kuchagua Viongozi Katika Zoezi la Uchaguzi Lililofanyika Jana. Viongozi Wa Nafasi za Juu Wapatikana Kuanzia Nafasi za Vitivo hadi Serikali ya Shirikisho
Mawakala Wa Wagombea Wakiwa Ndani Ya Kituo Tayari Kuhakikisha Hakuna Tatizo Katika Kura za wagombea Wao.
Mawakala Wa Wagombea Wakiwa Katika Kituo Kimoja wapo Kabla zoezi la Kupiga Kura za kuwachagua viongozi wa Serikali Ya Wanafunzi Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma kuanza
Mmoja Wa Wanafunzi Akidumbukiza Karatasi Ya Kupigia Kura Mara Baada ya Kuwachagua Viongozi Anaowataka Wamtumikie.
Wanafunzi Wakiwa Wanatumbukiza Karatasi Za Kupigia Kura Mara baada ya Kuchagua Viongozi Wanaowataka.
Wanafunzi Wakiwa Katika Foleni kwaajili ya kuchukua karatasi za kuchagulia Viongozi Katika Mchakato wa Kuwapigia Kura Wagombea Wanafasi za Uwakilishi Wa Shule(SCHOOL REPRENSETED), MEMBER OF PARLIAMENT (MP), Na CHAIRPERSON OF COLLEGES na UDOSO FEDERATION
Wakiulizana Ni Nani Tumpe Kura Zetu. Hapo Nadhani Walikua Wakishauriana Ni Nani wampe kura
Mara Nyingi Baada Ya Hapa Ndio Utata Huwa Unaanza Wa Kukataa matokeo.Msimamizi Wa Kituo Akiwa Anahesabu Kura Zote Zilizopigwa Kwaajili Ya Kuanza Kuhesabu Kura Za Mgombea Mmoja Mmoja.
Msimamizi Wa Kituo Akirudisha Kura Kwenye Sanduku Mara baada ya Kuhesabiwa. Na Mchakato Wa Kuhesabu Kura za Mgombea Mmoja Mmoja Ulianza.
Wanafunzi Wakiwa Nje Ya Kituo Cha Kupigia Kura Wakisubiri Matokeo Mara baada ya Muda Wa Kupiga Kura Kumalizika saa 11 jioni hapo jana.
Jana Wanafunzi Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma Walifanya Uchaguzi Katika Vitivo Vyote Vitano Kuwachagua Viongozi Wao. Hali Ambayo Ilileta Utata Katika Kitivo Cha Elimu Ambapo Mtu Mmoja Alnasidikiwa Kuumizwa Vibaya Na Wenzake katika Hali Ya Ushabiki.Mwanafunzi Huyo Aliweza Kufikishwa Hospitalini na Kupewa Matibabu pamoja Na Kushonwa Nyuzi.
Vilevile Wakati Wanafunzi Wa Kitivo Cha Sayansi Ya Jamii, Sanaa na Lugha Wakisubiri Matokeo ya Viongozi Hadi Saa Tisa Usiku Wanafunzi Waliweza Kushinikiza Tume Ya Uchaguzi Kutoa Matokeo Mapema huku Wengine wakisikika Wakisema "MKICHAKACHUA TUNAWAUWA" hayo ni baadhi ya Maneno yaliyokuwa yakisemwa mida ya saa nane usiku hali iliyopelekea kituo hiko kilichokua kikisubiri matokeo ya vituo vyote vya vitivo vyote yaweze kujumlishwa na kumtangaza mshindi wa waliokua Wakiwania Nafasi Ya Uraisi Wa Chuo Kizima.
Kufikai Mida ya Saa Tisa Usiku Tume Ya Uchaguzi Iliweza Kuwatangaza Wafuatao Kuwa Ndio Washindi katika Nafasi ya Uraisi Wa College na Uraisi Wa Chuo Kizima Cha Dodoma.
Mshindi Wa Uraisi Wa Kitivo Cha Sayansi Ya Jamii, Sanaa na Lugha Ni Mwakibinga Philipo Ambaye ameshinda Kwa Kura zaidi Ya 1000 huku wapinzani Wake akiwa na Kura zisizozidi 800
Na Katika Nafasi ya Uraisi Wa Chuo Kizima Ya Shirikisho (UDOSO FEDERATION) Nafasi hiyo Iliweza Kuchukuliwa Kwa Mara Ya Kwanza Ambapo haijawahi kutokea Katika Chuo Kikuu Cha Dodoma tokea Kuanzishwa Kwake Nafasi Ya Makamu Wa Raisi Wa Federation na Raisi Wa Federation Kuchukuliwa Na Wanawake.
Mshindi Wa Uraisi Wa federation Ni Miss Debora Huku Makamu Wake Ni Theresia Mtewele.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)