MAKAMU WA RAISI DK BILAL AWASILI UTURUKI JANA KUMWAKILISHA RAISI KATIKA MKUTANO WA UMOJA WA MATAIFA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MAKAMU WA RAISI DK BILAL AWASILI UTURUKI JANA KUMWAKILISHA RAISI KATIKA MKUTANO WA UMOJA WA MATAIFA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akiongozana na mkewe Mama Zakhia Bilal na baadhi ya viongozi alioongozana nao baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa ndege wa Ataturk jijini Istanbul jana, kwa ajili ya kumwakilisha Rais Jakaya kikwete katika Mkutano wa Umoja wa Matifa unaohusu maendeleo ya nchi maskini, Mkutano huo unaanza kesho na kumalizika Mei 13, 2011.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi Sundery ambaye ni Balozi wa Uturuki nchini Tanzania. Hii ni baada ya Dkt. Bilal kuwasili mjini Istambul jana.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akisalimiana na Msaidizi wa Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Modest Mero, baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Ataturk jijini Istambul jana. Makamu wa Rais yuko nchini Uturuki kumwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika mkutano wa Umoja wa Matifa unahusu maendeleo ya nchi maskini, Mkutano huo unaanza kesho na kumalizika Mei 13, 2011. Katikati ni Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akisalimiana na Dkt. Mbaraka Lijohiy.

Makamu wa Rais, akiwa katika picha ya pamoja na Dkt. Mbaraka Ljohiy, ambaye ni Mkurugenzi wa Plastic , Reconstructive, Esthetic Had and Microsurgeory (kulia) na mfanyabiashara aishie nchini Uturuki, Ally Kilumba baada ya kukutana nao jana alipowasili jijini Instanbul

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages