Askari 13 wa jeshi la polisi na raia 46 wamejeruhiwa vibaya baada ya lori lililokuwa limebeba mafuta kugonga kichwa cha treni na kupinduka wilayani Manyoni, Singida, Aprili 10, mwaka huu.
Ajali hiyo ilihusisha lori lenye namba za usajili T 483 BLM lililokuwa likitokea Dar es Salaam kuelekea mkoani Shinyanga likiwa na lita 40,000 za mafuta ya petroli na kichwa cha treni chenye namba 824 mali ya Shirika la Reli Tanzania (TRL).
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani Singida, Selina Kaluba aliyezungumza kwa njia ya simu akiwa eneo la tukio, alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa lori aliyegonga kichwa cha treni na kusababisha maafa makubwa.
Aidha, Kamanda Kaluba aliliambia Uwazi kuwa, baada ya lori hilo kugonga kichwa hicho cha treni na kupinduka lilimwaga mafuta hayo ya petroli lakini cha kushangaza wananchi wanaozunguka eneo hilo walikimbilia kwenda huko kwa ajili ya kutaka kuchota mafuta hayo.
Akiendelea kuelezea, kamanda huyo alisema baada ya kuona wananchi wanaiba mafuta aliagiza askari wa kutosha kwenda eneo la tukio kwa ajili ya kulinda usalama.
Kamanda Kaluba alisema kuwa, muda mfupi baada ya mafuta kuanza kumwagika, ghafla lori hilo liliwaka moto na watu zaidi ya 46 walijeruhiwa wakiwemo askari 13 wa jeshi la polisi waliofika eneo la tukio kulinda usalama.
Aidha alisema hadi sasa watu wanne kati ya majeruhi hao wamefariki dunia na wengine 46 wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Singida kwa matibabu.
Kamanda Kaluba amebainisha kuwa, lori hilo ni mali ya Mohamed Abed, 40, mwenye asili ya Kiarabu, mkazi wa Mkoa wa Shinyanga.
Dereva wa lori hilo aliingia mitini baada ya ajali hiyo kutokea na polisi wanaendelea kumtafuta.

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)