CCM WAFURAHIA KUONDOLEWA KWA MAKAMBA NA SEKRETARIETI NZIMA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

CCM WAFURAHIA KUONDOLEWA KWA MAKAMBA NA SEKRETARIETI NZIMA

WAFANYAKAZI wa CCM Makao Makuu Dodoma wamejipongeza kwa kula na kunywa kwa kile wanachosema ni kufurahia kuondolewa ofisini kwa
aliyekuwa Katibu Mkuu, Bw. Yusufu Makamba jambo walilokuwa wanalisubiria kwa muda mrefu.
Baadhi ya wafanyakazi hao waliokutwa na Majira katika maeneo mbalimbali ya starehe mjini Dodoma wakizungumza bila kutaka majina yao yaandikwe gazetini, walisema kwamba furaha yao hiyo imenogeshwa zaidi na kuondolewa kwa sekretarieti nzima ambayo ilikuwa mzigo mkubwa, sio kwa chama tu bali pia kwa watumishi wa chama.
Walisema uwajibikaji wa watumishi ulipungua kutokana na maamuzi binafsi ya Bw. Makamba ambayo kila mara yalitolewa bila kuzingatia taratibu za utumishi na ajira. Kwamba baadhi ya watumishi walihamishwa kibabe kwa amri yake kwa sababu binafsi.
“Kuondoka kwa uongozi wa Makamba kwetu ni sawa na kuzaliwa upya, ndio maana tuko hapa tukiburudika kwa furaha na kupongezana. Kuondoka kwao haikuwa kazi ndogo kwani tayari baadhi ya wajumbe walishapewa kiasi kikubwa cha pesa ili kukwamisha na kuhujumu uamuzi wa kuwaondoa madarakani,” alisema mmoja wa wafanyakazi hao.
Kwa Habari Zaidi   <<< BOFYA HAPA >>>

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages