TIMU ya Taifa Soka ya Wanawake ya (Twiga Stars), imefuzu kucheza fainali michezo ya Afrika (All Afican Games) inayotarajia kufanyika mwezi Septemba mwaka huu Msumbiji.
Twiga imefuzu na kutinga katika fainali hizo baada ya wapinzani wao waliokuwa wamepangwa katika kundi moja Sudani kujitoa.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa semina ya TBL Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah, alisema kuwa timu ya Twiga ilipangiwa kundi moja na Sudani ambapo ilikuwa icheze ilitakiwa kwenda Sudani Aprili 30 kwa ajili ya mchezo wa kwanza.
Aidha Angetile, alisema kuwa TFF imepokea taarifa kutoka Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) lililotoa tamko la kuipitisha Twiga kufuzu fainali hizo na kusema kuwa Sudan haitaweza kushiriki michuano hiyo na hivyo kuipa nafasi Twiga Stars kufuzu fainali hizo kwa mara ya kwanza.
"Kutokana na taarifa hizo sasa timu hiyo iliyokuwa imeanza mazoezi na kambi kwa ajili ya maandalizi hivi sasa itavunja kambi na TFF itaanza utaratibu wa kuwatafutia michezo ya kimataifa ya kirafiki kadhaa ili kuendelea kujiweka fiti kwa fainali hizo" alisema Angetile
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)