Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha nchini Rais wa Jamhuri ya Somalia Mhe.Sheikh Sharif Sheikh Ahmed muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo mchana.
Rais wa Somalia mhe.Sheikh Sharif sheikh Ahmed akikagua gwaride la heshima lililoandaliwa na jeshi la Wananchi wa Tanzania wakati wa mapokezi Yake baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo mchana.Picha na Freddy Maro-IKULU
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)