THOMAS KASHILILA: UTARATIBU WA KUTUNGA SHERIA KWA MAMBO YA JUMLA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

THOMAS KASHILILA: UTARATIBU WA KUTUNGA SHERIA KWA MAMBO YA JUMLA


Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Thomas Kashilila akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam katika Ofisi ndogo za Bunge.Picha na  Fadhili Akida
---
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo limetoa taarifa yenye lengo la kutoa habari kuhusu shughuli za Bunge kwa mujibu wa Katiba, Sheria, Kanuni na Taratibu mbali mbali zinazotumika kuendesha shughuli za Bunge.
Taarifa hiyo imelenga kujadili mchakato wa kutunga sheria kuanzia na mamlaka ya Bunge ya kutunga sheria pamoja na mchakato mzima kuanzia kutangaza, kuwasilisha, kujadili, kupitishahadi muswada kusainiwa na rais kuwa sheria na pia taarifa hiyo imezungumzia mamlaka ya Spika kusimamia shughuli za Bunge.
Taarifa hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam katika Ofisi za Bunge ambapo Katibu wa Bunge Dk. Thomas Kashilila amezungumza na waandishi wa habari kutoka vyombo mbali mbali hapa nchini.
Akizungumzia Mamlaka ya Bunge Dk. Kashilila amesema kwa mujibu wa Ibara ya 63 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepewa mamlaka ya Kuisimamia, Kufuatilia Utendaji na Kuishauri serikali ikiwa ni pamoja na Kutunga Sheria na Kupitia Mikataba ya Kimataifa.
Kuhusu Mchakato wa kutunga Sheria Dk. Kashilila amesema Utaratibu wa kutunga sheria umeainishwa katika Kanuni ya 80 – 93 ya Kanuni za Bunge (2007) ambazo zimeainisha utaratibu wa kuwasilisha miswada mpaka Bunge kupitisha miswada hiyo.
Katika Suala la Mamlaka ya Spika Katika Kazi za Bunge Dk. Kashilila amefafanua kuwa kwa mujibu wa Ibara ya 84 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1077, Spika ambaye huchaguliwa na wabunge kutoka miongoni mwa wabunge au mwa watu wenye sifa za kuwa mbunge, ndiye kiongozi wa bunge na atawakilisha bunge katika vyombo na vikao vingine vyote nje ya bunge.
Aidha kwa mujibu wa kanuni ya 5, Spika atawajibika kutilia nguvu kanuni zote za bunge, ambapo katika kutekeleza majukumu yake, Spika ataongozwa na Kanuni za Bunge na pale ambapo kanuni hazikutoa mwongozo, atafanyakazi kwa kuzingatia katiba, sheria nyingine za nchi, kanuni nyingine zilizopo, maamuzi ya awali ya Maspika wa Bunge na mila na desturi ya/za mabunge mengine yenye utaratibu wa kibunge unaofanana na utaratibu wa Bunge la Tanzania. 

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages