RAIS KIKWETE AMTEUA BW. CLEMENT MSHANA KUWA MTENDAJI MKUU WA SHIRIKA LA UTANGAZAJI TANZANIA (TBC) - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

RAIS KIKWETE AMTEUA BW. CLEMENT MSHANA KUWA MTENDAJI MKUU WA SHIRIKA LA UTANGAZAJI TANZANIA (TBC)



 Clement Mshana
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Clement Senzota Mwete Mshana kuwa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).
Taarifa iliyotolewa Ikulu, Dar es Salaam, leo, Jumatano, Aprili 27, 2011, na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Bwana George Yambesi inasema kuwa uteuzi huo unaanzia Alhamisi iliyopita, Aprili 21, mwaka huu, 2011.
Kabla ya uteuzi huo, Bwana Clement Senzota Mwete Mshana alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo).
Bwana Mshana anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bwana Dunstun Tido Mhando ambaye amemaliza muda wake wa utumishi kwa mujibu wa mkataba wake.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
27 Aprili, 2011

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages