SPIKA WA BUNGE ANNE MAKINDA: NAONGOZWA NA KANUNI ZA BUNGE NA SI KWA MATAKWA YA WABUNGE - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

SPIKA WA BUNGE ANNE MAKINDA: NAONGOZWA NA KANUNI ZA BUNGE NA SI KWA MATAKWA YA WABUNGE


Spika wa Bunge Anne Makinda akizungumza Bungeni mjini Dodoma leo.
--
Na.Mwandishi wetu,Dodoma.
Spika wa Bunge Anne Makinda amewapasha wabunge kuwa anaongozwa na kanuni na si kwa matakwa ya wabunge na kuwa hajafungwa kitambaa usoni kiasi cha kushindwa kufahamu anachokifanya pindi anapoongoza vikao vya Bunge.

Hatua ya Spika Anne kutoa kauli hiyo imekuja kufuatia baadhi ya wabunge kusimama na kuomba mwongozo wa Spika wakati akiendelea kuzungumzia masuala mbalimbali bungeni leo.
Kabla ya wabunge hao kusimama kuomba mwongozo Mbunge wa Arusha Mjini Mh. Godbless Lema (Chadema) akihoji jina lake kutokuwepo katika orodha ya wabunge waliomuuliza maswali Waziri Mkuu  Mh. Mizengo Pinda, amesema kuwa aliwahi kujiandikisha kwa kuuliza swali, lakini anashangaa hakuweza kupata fursa ya kufanya hivyo.

Akijibu hoja hiyo Spika Anne amesema idadi ya walioomba kumuuliza maswali Waziri Mkuu ni kubwa na kwamba alichagua wachache kulingana na jinsia, vyama na majimbo.Hata hivyo, baada ya kujibu hoja hiyo wabunge takribani watano waliwasha vipaza sauti kuomba mwongozo wa Spika, hatua iliyomlazimu Anne kusimama na kusema kuwa hawezi kuongozwa na wabunge na kuwa yeye ndiye anayeongoza vikao.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages