OFISA MTENDAJI WA KATA YA RUAHA MANISPAA YA IRINGA AJIUA BAADA YA KUTUHUMIWA KWA UFISADI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

OFISA MTENDAJI WA KATA YA RUAHA MANISPAA YA IRINGA AJIUA BAADA YA KUTUHUMIWA KWA UFISADI

Na Francis Godwin, Iringa

BAADA ya kutuhumiwa kwa ufisadi na kuripotiwa na vyombo mbali mbali vya habari ikiwemo TBC na ITV na magazeti mbali mbali ,Ofisa mtendaji wa kata ya Ruaha, manispaa ya Iringa, Nuhu Feruzi (40) ameamua kujiua kwa kunywa sumu usiku wa kuamkia leo akikwepa malalamiko ya wananchi ya kumwita ni fisadi.


Kabla ya kuchukua uamuzi wa kujiua wananchi wa kata hiyo,walionyesha kutokuwa na imani nae kiasi cha kuamua kuifunga ofisi ya Afisa mtendaji huyo, baada ya kudai taarifa ya mapato na matumizi ya fedha za kata hiyo ikiwemo sh mil 24.6 ya rusuku, kwa zaidi ya siku tatu, bila mafanikio hali iliyosababisha ofisi ya Mkurugenzi wa manispaa hiyo kuingilia kati na kuamua kumsimamisha kwa muda ili kupisha uchunguzi.

Kaim afisa mnadhimu wa jeshi la Polisi Mkoani Iringa, Hamfrey Saganya alisema kuwa afisa mtendaji huyo, alikutwa akiwa amekufa chumbani kwake, baada ya kunywa sumu ambayo haijajulikana aina yake, katika maeneo ya Mwangata, Manispaa ya Iringa.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages