AKUTWA HOI AKIUCHAPA USINGIZI KATIKA DIMBWA LA MATOPE SINZA DARAJANI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

AKUTWA HOI AKIUCHAPA USINGIZI KATIKA DIMBWA LA MATOPE SINZA DARAJANI

Wananchi wakazi wa Sinza Darajani Kata ya Sinza D jijini Dar es Salaam, wakimuangalia kijana ambaye hakuweza kufahamika jina lake, aliyekutwa amelala kwenye uwanja wa mpira wa Darajani leo asubuhi huku akiwa bado anapumua.

Baada ya kufika eneo hilo wakazi hao waliweza kusikia sauti ya kijana huyo akiomba msaada wa kupewa maji ya kunywa na alipoulizwa sababu za kuwa katika hali hiyo huku akiwa na majeraha kibao na akiwa amelala katika matope alijibu kuwa alitoka kuiba maeneo ya Tandale na ndiko alipopewa kipigo cha mbwa mwizi na kufanikiwa kutimka ili kujiokoa na alipofika maeneo hayo alizidiwa na kuwanguka, lakini baada tu ya kutoa jibu hlo hakuweza tena kuzungumza wala kufumbua macho hadi Sufianimafoto anatoka eneo hilo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages